Serikali ya Urusi, imewafungulia mashtaka watu wanne wanaodaiwa kufanya shambulizi katika ukumbi wa Crocus City Hall jijini Moscow usiku wa kuamkia Machi 23, 2024 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 130 karibu na jiji la Moscow.

Wamefunguliwa mashtaka ya ugaidi katika Mahakama ya Wilaya ya Basmanny mjini Moscow ambapo huenda wakakabiliwa na hukumu ya maisha jela, lakini wataendelea kubaki kizuizini hadi Mei 22, 2024 kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo inayowakabili.

Taarifa ya Mahakama imewataja washtakiwa hao kuwa ni Dalerzdzhon Mirzoyev (32), Saidakrami Rachabalizoda (30), Shamsidin Fariduni (25) na Mukhammadsobir Faizov (19) na wawili kati yao walikiri kuhusika na shambulizi hilo.

Hata hivyo, watu haio walionesha dalili za kuwa hoi kwa kipigo, huku kukiwa na mashaka kuhusu uhuru waliokuwa nao wakati wakijibu maswali waliyokuwa wakihojiwa.

Hersi Said: Tunakwenda Nusu Fainali
Sofyan Amrabat kurudi Italia