Kiungo wa Manchester City, Joao Cancelo ambaye anacheza kwa mkopo FC Barcelona amesema Kocha Pep Guardiola alisema uongo juu yake, aliruhusiwa kuondoka kutokana na kiwango chake na tabia zake.

Cancelo ambaye alijiunga na Bayern Munich dirisha la majira ya kiangazi mwaka juzi kwa mkopo akitokea Man City kabla ya kutua Barca msimu huu, amesema Man City na Pep hawana shukrani kwake.

“Waliongopa, sijawahi kuwa mtu mbaya kwa wachezaji wenzangu ama timu kwa jumla, unaweza kuwauliza Nathan Ake au Rico Lewis, sijawahi kujiona bora ama mkubwa zaidi yao, kilichosemwa ni mtazamo tu wa kocha mwenyewe.”

“Nafikiri Man City wamekosa shukrani kwangu kwa kusema maneno hayo, kwa sababu nimekuwa mchezaji muhimu kwao katika miaka yote ambayo nimekuwa nikihudumu kwenye kikosi chao, kila siku nilikuwa nikijitolea kwa ajili ya timu na kupambana hadi dakika za mwisho, nakumbuka siku niliyokabwa halafu kesho yake nikachecza mechi dhidi ya Arsenal pale Emirates.”

“Hivi ni vitu ambavyo huwezi kusahau, nilimuacha mke wangu na mtoto wangu nyumbani kwa ajili ya timu, watu wanamuamini Guardiola ni kwa sababu ana nguvu kuliko mimi, mimi daima huwa napenda kusema ukweli na kuchunga sana maneno yangu, siwezi kuongopa ningependa maisha yaendelee na muda mwingine natamani kila kitu kingekuwa sawa nikaendelea kucheza hapo kwa sababu ni sehemu niliyokuwa nainjoi sana kucheza.”

Hivi karibuni alisema hana mpango wa kurudi tena Man City na badala yake atasaini mkataba wa kudumu na Barca au ikishindikana ataangalia timu nyingine ya kuichezea.

Mgombea wa Upinzani aukaribia ushindi Senegal
Dkt. Nchimbi: Umoja wa Kitaifa ni maisha ya Watu