Kiungo wa Real Madrid, Aurelien Tchouameni, ameeleza kusikitishwa na uamuzi wa klabu hiyo kuwazuia wachezaji wake waandamizi kushiriki michuano ya Olimpiki msimu huu.

Tchouameni alikuwa na mpango wa kuiwakilisha Ufaransa katika mashindano ya soka ya wanaume katika ardhi ya nyumbani kama mchezaji aliyezidi umri, huku mchezaji mwenzake, Eduardo Camavinga pia akistahili.

Kylian Mbappe ambaye anatarajiwa kuwa mchezaji wa Madrid Julai mwaka huu, ni mchezaji mwingine ambaye Olimpiki ni matarajio yake.

“Ni wazi, kucheza katika Michezo ya Olimpiki, katika nchi yako, ni jambo la aina yake. Si jambo ambalo labda tunaweza kurudia katika maisha yetu, lakini Real Madrid ni mwajiri wetu,” alisema Tchouameni akiwa kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Ufaransa.

“Tangu wakati Real Madrid ilipoamua, nadhani hatuna mengi ya kusema. Mbali na hilo, kila mtu anajua kwamba si lazima kutofautiana na mwajiri wako katika maisha ya kila siku.

Ukweli ni kwamba tungependelea. Hilo halitawezekana lakini tutakuwa wa kwanza kuiunga mkono Ufaransa.”

Katika soka ya wanaume, Olimpiki ni mashindano ya vijana chini ya miaka 23, lakini kila nchi inaruhusiwa kuchagua hadi wachezaji watatu wakubwa.

Mbappe mwenye umri wa miaka 25 na Tchouameni mwenye miaka 24, wangehesabiwa katika nafasi hiyo, huku Camavinga akiwa bado na miaka 21.

Lakini kwa kuwa wachezaji kama Lionel Messi na Neymar ni miongoni mwa wachezaji wa hadhi ya juu walioshinda medali za dhahabu kufikia sasa karne hii, inazidi kuwa ya kifahari.

Mashindano ya kandanda ya Olimpikiya 2024 yataanza Julai 25 hadi Agosti 10, yakianza siku tisa tu baada ya fainali ya Euro 2024.

Jose Mourinho kupiga kazi Afrika
Miundombinu bora hurahisisha huduma za afya - Dkt. Biteko