Majadiliano kati ya Kocha kutoka nchini Ureno Jose Mourinho na Shirikisho la Soka nchini Cameroon ‘FECAFOOT’ yanaonekana kupiga hatua kubwa kwa ajili ya kocha huyo kuinoa ‘The Indomitable Lion’.

Cameroon imekuwa katika mchakato wa kumsaka Kocha Mkuu wa Mpya wa Kikosi chao cha Taifa, baada ya kuachana na Kocha mzawa Rigobert Song mwezi uliopita.

José Mourinho anatafuta changamoto mpya baada ya kuachana na klabu ya AS Roma ya Italia Januari 2024, kufuatia mfululizo mbaya wa matokeo ligi kuu Italia.

‘The Special One’ anaweza kuchukua mikoba ya kuinoa timu ya taifa ya Cameroon endapo mazungumzo yatakwenda vizuri na Cameroon.

Ingawa Mourinho anapewa nafasi kubwa ya kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa mshahara unaweza kuwa kikwazo kati yake na Cameroon.

Waandishi wawili wafariki kwa ajali Lindi
Katazo la Real Madrid lamsikitisha Tchouameni