Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Rufiji (Pwani), Protas Mutayoba amethibitisha kutokea kwa ajali ya Gari dogo aina ya Toyota Sienta iliyogongana na Lori aina ya Eicher iliyouwa Waandishi wawili wa Habari, katika eneo la Nyamwage Rufiji usiku wa kuamkia leo Machi 26, 2024.

Waandishi hao, Abdalla Nanda (Chanel Ten – Lindi) na Josephine Kibiriti – Sahara Media Group), walikuwa wakirejea Mkoani Lindi wakitokea jijini Dar es Saalam kwenye Semina iliyokuwa imeandaliwa na Mtandao wa Kijinsia Nchini – TGNP, ambapo majeruhi mmoja amelazwa Kituo cha Afya Ikwiriri kwa matibabu.

Kamanda Mtayoka amesema, chanzo cha ajali hiyo iliyotokea majira ya saa sita na nusu usiku bado hakijafahamika na Dereva wa Gari Lori lililokuwa likitokea Lindi, alikimbia kusikojulikana baada ya tukio na anatafutwa ili kueleza nini kilitokea.

Amesema, “imetokea ajali ya magari kugongana, nagari hayo ni ile iliyokuwa imebeba Waandishi ikitokea Dar es Salaama kuelekea Lindi na Lori aina ya Eicher iliyokuwa ikitokea Lindi kuelekea Dar es Salaam, yalivyofika katika eneo hilo yakawa yamegongana lakini bahati mbaya Dereva wa Roli amekimbia na tunaendelea kumtafuta sababu yeye anaweza kutuambia kitu gani kilitokea.”

KMC FC kucheza kimataifa 2024/25
Jose Mourinho kupiga kazi Afrika