Polisi wa Argentina wanachunguza vitisho vya kifo vilivyotolewa kwa familia ya mshambuliaji Angel Di Maria nyumbani kwao Roasario.

Wafanyakazi kwenye nyumba ya staa huyo mshindi wa Kombe la Dunia na Argentina mwaka 2022, walisema walikutana na ujumbe uliokuwa na vitisho vya vifo kama ataendelea kucheza kwenye moja ya klabu katika mji wa Rosario.

Winga huyo mwenye umri wa miaka 36 wa Benfica ya Ureno hivi karibuni alisema anaweza kurejea kucheza kwenye klabu yake ya utoto ya Rosario Central. Kwa sasa yuko Marekani na timu ya taifa ya Argentina.

“Vitisho kama hivi vinasababisha usumbufu mwingi kwenye jamii na hilo ndio lengo lake, kufanya wananchi wawe na hofu, kuwatisha watu muhimu kwenye jamii,” alisema Esteban Santantino, anayefanya kazi kwenye vyombo vya usalama katika mji wa Rosario.

Vyombo vya habari vinasema malengo ya vitisho hivyo bado hayako wazi, ingawa Polisi walishindwa kukataa taarifa zozote za uchunguzi.

Di Maria alianza kwenye mchezo wa jana wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Costa Rica kwa mujibu wa kocha wa timu hiyo, Lionel Scaloni.

“Di Maria anafahamu tuko nyuma yake kwa chochote atakachohitaji. Kitu muhimu ni kwamba alicheza, hicho kitamfanya apate faraja kidogo.

Rosario imekumbwa na matukio ya vurugu nyingi miongoni mwa magenge yanayohusika na uuzaji wa dawa za kulevya. Mauaji ya watu kwenye mji huo ni watu 22 kwa 100,000.

Job: Tunaifahamu Mamelodi Sundowns
Tanzania yamuahidi ushirikiano Rais mteule Senegal