Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuahidi ushirikiano wa karibu Rais mteule wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye katika kuimarisha uhusiano kwa manufaa ya pande zote.

za Rais Samia, ameahidi hayo kupitia chapisho lake kwenye kurasa rasmi za mitandao ya kijamii z Rais akieleza kuwa ni matarajio yake kuendelea kufanya kazi pamoja, ili kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Senegal.

Ameeleza kuwa, “nawasilisha pongezi zangu za dhati kwa Mheshimiwa Bassirou Diomaye Faye, Rais Mteule wa Jamhuri ya Senegal, kwa ushindi wako katika uchaguzi wa urais wa 2024 wa Senegal; na watu wa Senegal kwa uchaguzi wa amani.”

Bassirou Diomaye Faye (44), amekuwa Rais mwenye umri mdogo zaidi wa Senegal, akizaliwa Machi 25, 1980 eneo la Thiès.

Di Maria atishiwa maisha Argentina
Kibadeni amkataa Manula dhidi ya Al Ahly