Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Abdallah Pazi Dullah Mbabe amesema kuwa hakutegemea kupoteza pambano lake dhidi ya Callum Simpson hivyo anataka pambarno la marudiano ili asahihishe makosa yake.

Mbabe alicheza dhidi ya bondia Simpson raia wa Uingereza pambano la kimataifa la Raundi 10 lililofanyika kwenye ukumbi wa 02 Arena jijini London na kupoteza kwa KO Raundi ya nne baada ya kuokolewa na mwamuzi.

Dulla Mbabe amesema matokeo hayo hayajamfurahisha kwani lengo lilikuwa ni kupata ushindi na kujiweka kwenye nafasi za juu kwenye viwango vya ubora.

“Najua mashabiki wangu hawajafurahishwa na matokeo haya, mimi pia yananiumiza kutokana na maandalizi mazuri niliyofanya lakini ndio matokeo ya mchezo nimeyakubali.

“Narudi kuangalia pambano langu kwa umakini ili kuona wapi niliteleza nikashindwa kurudi na ushindi nyumbani, lakini pia mwalimu wangu atapata nafasi ya kuona wapi anapaswa kuongeza,” amesema Dulla Mbabe

Babati mwenyeji fainali Kombe la Shirikisho
Kwa ajili ya burudani: Serikali yaruhusu uvutaji Bangi