Ni Taifa kubwa la Umoja wa Ulaya, likifahamika kama Ujerumani, rasmi limehalalisha matumizi ya bangi kwa ajili ya kujiburudisha licha ya pingamizi kali kutoka kwa Wanasiasa wa upinzani na Wanaharakati wa masuala ya Afya wanaosema hatua hiyo itawaathiri Vijana na sasa inakuwa nchi ya tatu kufanya hivyo baada ya Malta na Luxemburg.

Hatua hiyo inaungwa mkono na Wizara ya afya ambayo inasema itasaidia kuzuia masoko yasiyo rasmi yanayouzwa bangi, yanayozalisha Euro Bilioni 4 kila mwaka, huku Watu wazima wakiruhusiwa kubeba hadi gramu 25 pamoja na kulima hadi miche mitatu, ingawa ni marufuku kuvuta bangi ndani ya mita 100 kwenye maeneo ya michezo na shule.

Ni rasmi sasa kuanzia Julai mosi 2024, Serikali ya Taifa hilo imesema watu wazima wataruhusiwa kununua bangi kutoka kwa vilabu vya watu wasiozidi 500, ambao kila mmoja atapata hadi gramu hamsini za bangi kila mwezi.

Hata hivyo, Wanaharakati wamezidi kufafanua kuwa hatua hiyo itaathiri mfumo wa maisha kwa watumiaji, ingawa imekuwa ni habari njema kwa watumiaji wa mmea huo wanaokadiriwa kufikia Milioni 4.5

Dullah Mbabe afunguka kuchakazwa England
Mwanafunzi mjamzito wa miezi tisa ajinyonga