Mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu, Faith Charity Makhulu (19), ambaye alikuwa mjamzito, anadaiwa kujiua katika mtaa mmoja mjini Kericho, katika mtaa wa Site and Service.

Kulingana na ripoti ya polisi, Mwanafunzi huyo wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Mount Kenya bewa la Kericho, alikuwa na mimba ya miezi tisa mpaka anafikia uamuzi huo.

Inasemekana kuwa alitumia kamba ya manila kujinyonga katika makazi ya familia yake Ijumaa (Machi 29, 2024) na mwili wake ulikutwa na alama za kamba shingoni na hakuna ujumbe wowote alioacha marehemu huku Polisi wakianza uchunguzi.

Kaunti za Bomet, Narok na Kericho ndizo zinaongoza kwa visa vinavyohusisha na Wanafunzi wa taasisi mbalimbali za masomo kujinyonga, ambapo Mhadhiri wa zamani wa Chuo Kikuu cha Moi, Dkt. Langat amesema vijana wengi wanakabiliwa na changamoto za kisaikolojia na wanahitaji kusaidiwa.

Kwa ajili ya burudani: Serikali yaruhusu uvutaji Bangi
Lewandowski akataa mamilioni Saudi Arabia