Serikali ya Taiwan imesema idadi ya watu waliofariki katika tetemeko la ardhi imefikia tisa, huku Mamlaka za Uchina zikisema mbali na janga hilo hilo lenye ukubwa wa 7.4 katika kipimo cha Richter kutokea pia inatahadharisha juu ya kutokea kwa tsunami na kwamba wapo tayari kutoa msaada wa maafa.

Pwani ya mashariki ya Uchina iko kilomita 180 (maili 111) kutoka Taiwan, na inadaiwa kuwa licha ya uhusiano wa Mataifa hayo kutia shaka wakati Taiwan ikijiona kuwa nchi huru huku Beijing ikisema ni jimbo lililojitenga na ambalo siku moja litakuwa sehemu ya nchi.

Hata hivyo, saa moja kabla ya tetemeko la ardhi, Wizara ya Ulinzi ya Taiwan ilikuwa imetoa taarifa ya kila siku ikibainisha kuwa ndege 20 za kijeshi za China zilivuka katika eneo lake la ulinzi wa anga katika muda wa saa 24 zilizopita.

Shirika la Kitaifa la Zimamoto la Taiwan limesema watu 711 wamejeruhiwa katika tetemeko hilo huku watu 77 wakiwa bado wamenasa kwenye vifusi ambapo majengo mengi yameporomoka huko Hualien na ilitokea mitetemeko tisa yenye ukubwa wa 4 au zaidi.

Alexander isak kupigwa pini Newcastle Utd
Ahmed Ally achefukwa, afunguka safari ya Afrika Kusini