Wanawake wawili wanahofiwa kufa maji na miili yao bado haijapatikana baada ya Mtumbwi waliokuwa wakisafiria ili kujiokoa na mafuriko kupinduka huko Kata ya Katindiuka Halmashuri Mji Ifakara Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro.

Akithibitisha tukio hilo, Diwani wa Kata ya Katindiuka, Tatu Njegeya amesema tukio hilo limetokea Machi 4, 2024 na kuwataja waliopoteza maisha kuwa ni Ratifa (35-40) na Lilian Pazi (30).

Amesema, jitihada za kuitafuta miili ya Wanawake hao bado zinaendelea na kwamba zoezi hilo litahusisha Mitumbwi mitatu.

Kaimu Mkurugenzi Halmashuri Mji Ifakara, Godwin Mukaluka akiambatana na Kamati ndogo ya maafa Wilaya hiyo wamefika nyumbani ilipo misiba hiyo na kutoa pole huku wakiwataka wananchi kuhama haraka maeneo yote hatarishi na watakaokaidi nguvu ya ziada itatumika.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Dunstan Kyobya amesema Serikali inaendelea kutoa msaada wa chakula kwa kutumia usafiriri wa Helkopta ya Jeshi la Wananchi – JWTZ, na kwamba mpaka sasa  kimeripotiwa kifo cha mtu mmoja katika eneo hilo.

Serikali kuongeza vituo tiba Saratani ya mionzi
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Aprili 6, 2024