Abel Paul, Jeshi la Polisi – Namanga Arusha.

Jeshi la Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa Mifugo kwa kushirikiana na Wananchi wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili wakitorosha mifugo 514 Kwenda Nchi Jirani, kwa kutumia vibali vya kampuni isiyohusika na Mifugo.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa Mifugo Nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP. Simon Pasua amesema Aprili 6, 2024 katika Wilaya ya Longido Mkoa wa Arusha waliwakama watu hao waliokuwa wakiitorosha kwenda nchi Jirani.

Amesema, majina ya Watuhumiwa hao yamehifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi huku akiwaomba Wananchi kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na utoroshaji na kukiuka taratibu za uuzaji wa Mifugo Nchini.

SACP Pasua amesisitiza na kuwataka Wananchi kufuata taratibu za uuzaji wa mifugo, ili kutokukumbana na mkono wa sheria na kulikosesha mapato Taifa huku akisema Jeshi hilo litaendelea kuwakamata wale wote watakao kiuka taratibu.

Nao baadhi ya Wafanyabiashara wa mnada huo wa mpakani Namanga wamewaomba Wananchi wenzao kufuata taratibu zilizopo, ili kutokukumbana na mkono wa sheria pindi wanapotaka kusafirisha mifugo yao nje ya nchi.

Daktari wa Mifugo Mnada wa Mpakani Namanga Longido Mkoani Arusha amewataka wafanya biashara kufuata taratibu huku akiwaomba wafanya biashara hao kufika na vibali vilivyo kamilika ili kuondoa usumbufu na wasimamizi wa Mnada huo.

KARUME DAY: Mambo mawili muhimu ya kukumbukwa
Shaka: Imani zetu za dini ziendelee kutuunganisha