Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Twaha Kassim maarufu Twaha Kiduku anatarajia kupanda ulingoni siku ya kesho kuzipiga dhidi ya bondia Harpeet Sigh Raia kutoka nchini India.

Katika kuelekea pambano hilo litakalofanyika ukimbi wa Tanzanite Mjini Morogoro  mabondia hawa wamepima uzito na afya wakitekeleza sheria na kanuni za mchezo wa ngumi, baada ya zoezi hili kila mmoja amejidhatiti kung’ara katika pambano hilo.

Nao baadhi ya mashabiki wa Twaha Kiduku wamesema wao wanaimani na bondia kwani awezi kuwaangusha tena amejifunza kutokana na makosa  hivyo wana Morogoro wanamtakia  ushindi kwenye pambano hilo.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Aprili 11, 2024
NEC sasa ni Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi