Kwenye Picha ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na waliokuwa walinzi wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine wakati wa Kumbukumbu ya miaka 40 tangu kifo chake, iliyofanyika Monduli mkoani Arusha Aprili 12, 2024.

Kulia ni aliyekuwa Mlinzi Mkuu Abihudi Michael Luila aliyekuwa gari ya nyuma wakati ajali inatokea na kushoto Mlinzi wa zamu Yusto Chuma ambaye alikuwa gari moja na Hayati Sokoine. Chuma wakati huo naye alijeruhiwa vibaya sana na kulazwa chumba cha wagonjwa mahututi kwa siku 14.

Hayati Sokoine alifariki dunia Aprili 12, 1984 kwenye ajali ya gari iliyotokea Wami Dakawa Wilayani Mvomero, Mkoani Morogoro.

Dkt Chimbi: Tutasimamia misingi ya utawala bora
DC Malisa aingilia kati mgogoro Soko la Wamachinga Old Airport