Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi – CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amesema moja ya sera muhimu za chama tawala ni pamoja na Serikali zake zote mbili, kusimamia na kuamini katika misingi ya utawala bora.

Akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM mjini Mpanda, Dk Nchimbi amesema chama hicho kina wajibu wa msingi wa kusikiliza kero za wananchi kwa kufuata utawala wa sheria bila kuingilia mashauri yaliyoko mahakamani.

Amesema, “mambo tutakayoyashughulikia kama kero, hatutagusa yaliyoko mahakamani. Huo ndiyo utaratibu wa utawala bora. Mojawapo ya sera muhimu sana za CCM ni kusimamia utawala bora. Wakati wote wajibu wetu utakuwa kuzihamasisha mahakama zetu zitende haki bila kuziingilia katika uamuzi wake. Nchi inayotaka kufanikiwa lazima isimamie utawala bora.”

Aidha, Balozi Nchimbi ametoa wito kwa wana-CCM kuendelea kuwa mstari wa mbele kueleza masuala mbalimbali yanayoyotekelezwa na Serikali kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM bila haya, huku akisisitiza kuwa chama hicho tawala kitaendelea kuisimamia Serikali.

Wazimbabwe watua nchini kujifunza mfumo wa NeST
Habari Picha: Rais na Walinzi wa Hayati Sokoine