Swaum Katambo – Katavi.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi- CCM, Itikadi Uenezi na Mafunzo, Amos Makala amesema wametumia njia nzuri isiyozusha tafrani kusikiliza kero za Wananchi wa Mkoa wa Katavi, huku akiitaja njia hiyo kuwa ni ya kisayansi isiyo na kero.

Makala ameyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Kashaulili, katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Emmanuel Nchimbi na kudai kuwa wataendelea kutumia mfumo huo hata kwa mikoa iliyobaki ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Ruvuma.

Amesema, hawataishia kusikiliza kero pekee bali hata kutoa majawabu ya kero hizo kwa Wananchi.

Hata hivyo, Makala ametoa wito kwa Wananchi kujitokeza pindi viongozi wa Serikali ngazi ya Mkoa, Wilaya na Halmashauri wanapo tangaza kusikiliza kero zao na si kusubiri Viongozi wa Kitaifa.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Aprili 15, 2024
IGP Wambura asisitiza malezi, ulinzi kwa Watoto