Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura amewataka wazazi na walezi nchini, kuendelea kuimarisha suala la malezi bora ndani ya familia kwa kutimiza wajibu wao, hususani katika malezi na ulinzi wa mtoto.

IGP Wambura ametoa kauli hiyo hii leo Aprili 14, 2024 aliposhiriki adhimisho la Misa Takatifu Parokia Kuu ya Kristo Mfalme Jimbo Katoliki Moshi mkoani Kilimanjaro.

Amesema, wazazi wana wajibu wa kuhakikisha mtoto anafikia malengo yake ya kuja kulitumikia Taifa katika nafasi mbalimbali za uongozi, hivyo ikitokea mzazi au mlezi kushindwa kutimiza wajibu huo ni kosa mbele za MUNGU.

Makalla: Tunasikiliza kero kisayansi bila taharuki
Mvua yakata mawasiliano Barabara ya Mpanda, Kigoma