Swaum Katambo, Mpanda – Katavi.

Mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo Aprili 14, 2024 katika maeneo mbalimbali ya mji wa Mpanda, imesabisha madhara ikiwemo kufurika kwa Daraja la Misunkumilo lililopo mjini Mpanda Mkoani Katavi hali iliyopelekea kukatika kwa mawasiliano ya Barabara kati ya Mpanda na Kigoma.

Hata hivyo baadhi ya nyumba zilizopo Kata ya Misunkumilo ambazo idadi yake bado haijafahamika zimezingirwa na maji ingawa hakuna taarifa za uharibifu, majeruhi wala vifo.

Bado hakuna taarifa kamili iliyotolewa kuhusu ukubwa wa madhara yaliyosababishwa na Mvua hiyo, ingawa tayari Mamkala mbalimbali za Serikali zipo eneo la tukio.

 

IGP Wambura asisitiza malezi, ulinzi kwa Watoto
Israel yajipanga kulipa kisasi, Marekani yapinga