Wadau wa zao la Mnazi katika Kaunti ya Kilifi Nchini Kenya, wamejumuika na wauza Pombe ya Mnazi katika maandamano kuishinikiza serikali kuondoa vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Kitega uchumi chao.

Wadau hao, wanasema vikwazo vilivyowekwa na Serikali vinalemaza biashara zao, hivyo kujikuta katika wakati mgumu kumudu maisha kwani asilimia kubwa ya pato lao linategemea biashara ya zao hilo.

“Serikali imetupangia muda kiduchu wa kufanya kazi, hii haitafaa kwani hata mapato yatakuwa kidogo watuache tufanye kazi kama ni ushuru tunalipa na hatujawahi haribu cha mtu shida ipo wapi, tunajitafutia na tuna familia,” alisema mmoja wa waandamanaji Njoroge Kimath.

Wafanyabiashara hao waliofanya maandamano ya amani, wanasema muda uliowekwa wa kuuza pombe hiyo kuanzia saa kumi na moja jioni hadi saa tano usiku hautoshi na wanataka kuachwa huru au wapangiwe muda rafiki.

MAKALA: Mr. Bean: Jiwe lililokataliwa na Waashi
Mvua: 19 wafariki kwa Maporomoko ya udongo