Johansen Buberwa – Kagera.

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera, Faris Burhan amewaasa Vijana Mkoani humo hususani Maafisa usafirishaji maarufu kama Bodaboda, kuendelea kuwa wavumilivu wakati Serikali ikiendelea na maboresho ya sera ya mikopo.

Mikopo hiyo ni ile inayotolewa kwa Vijana, Wanawake na Watu mwenye Ulemavu, ambayo ilisitishwa naSerikali kutokana na baadhi ya vikundi kukopa fedha bila kurejesha kwa Wakati.

Burhan aliyasema hayo wakati akiongea na Wananchina Maafisa Usafirishaji hao wa kata ya Kabindi iliyopo Wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera katika ziara yake ya kikazi ya siku 16 ambayo ameianza katika Wilaya ya Biharamulo.

Bodaboda walia na mikataba kandamizi
Marekebisho Sheria za Habari; Kamati Zanzibar yaongeza kasi ufuatiliaji