Johansen Buberwa – Kagera.

Maafisa usafirishaji maarufu kama Bodaboda wa Kata ya Kabindi iliyopo Wilayani Biharamulo Mkoani Kagera, wameiomba Serikali kuwawezesha kupata mikopo ya Pikipiki za gharama nafuu, ili kuwanusuru na changamoto ya Pikipiki za mikataba kandamizi.

Ombi hilo wamelitoa kupitia kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi – CCM, Mkoa wa Kagera na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa, Faris Burhani katika mkutano wa hadhara wakati akizindua ziara ya kamati ya utelezaji ya siku 16 Mkoani Kagera.

Akiijibu ombi hilo, Mwenyekiti Faris amesema Serikali ilisitisha mikopo hiyo kwa lengo la kufanya maboresho ya sera mpya ya ukopeshaji ili ikiwezekana mikipo hiyo itolewe kwa kila kijana mwenye sifa na kwamba muda muafaka ukifika mikopo hiyo itolewa kwa usawa huku akiagiza vijana kupewa kipaumbele.

Ziara ya Kamati ya utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Kagera imezinduliwa april 14, 2024 Wilayani Biharamulo, ikiwa na lengo la kuhamasisha Vijana kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Parimatch yamtambulisha Haji Manara ‘El Bugati’
Sera mpya ya Mikopo kuwanufaisha Vijana