Mamlaka ya Maji jijini Dodoma – DUWASA, imesema sababu zinazochangia baadhi ya maeneo ya jiji hilo ikiwemo Ilazo na Ntyuka kuwa na uhaba wa maji licha ya kuwa na miundombinu bora, ni ongezeko la mahitaji ya watu.

DUWASA imesema maeneo hayo ambayo chanzo chake kikuu ni Tanki la Nzuguni, imekuwa kwenye changamoto hiyo hasa baada ya maeneo mengine kuunganishiwa Maji kutoa chanzo hicho.

Kutokana na tatizo hilo, imesema inapambana kuongeza msukumo wa maji kutoka eneo lililo na msukumo mdogo, hatua ambayo pia bado haijaanza ikitumainia kwamba itaondoa tatizo, njia ambayo licha ya kuwa ni za muda mfupi lakini zimeonesha mafanikio.

Aidha, imekiri kwamba uhalisia wa maji yanayozalishwa hauendani na mahitaji kwani imekuwa ikizalisha asilimia 52 pekee ya kile kinachotakiwa na kuendelea kufanya uwepo wa mgao wa maji jijini humo.

Hata hivyo, imesema Mradi wa ujenzi wa bwawa la Fakwa ambalo usanifu umekamilika utaondoa kikwazo hicho kabla ya mtandao wa Maji kutoka Ziwa Victoria kufika katika Makao Makuu hayo ya nchi.

Ubora: TBS hutenga Mil. 250 kuhudumia Wajasiriamali wadogo
Maporomoko ya udongo yauwa 12 DRC