Takriban watu 12 wamefariki na wengine zaidi ya 50 hawajulikani walipo kutokana na athari ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Nchini DRC, zilizosababisha maporomoko ya udongo wakati baadhi ya raia wakiendelea na shughuli zao katika eneo la Mto Kasai.

Maporomoko hayo ya ardhi pia yalitokea katika Wilaya ya Dibaya Lubwe, iliyopo Jimbo la Kwilu na yaliwadhuru watu waliokuwa wakifua nguo na wengine waliokuwa katika boti ambayo ilikaribia kutia nanga, ambapo Gavana wa muda wa mkoa, Felicien Kiway alisema miili 12 imetolewa kwenye vifusi.

“Waliokufa ni Wanawake tisa, Wanaume watatu na mtoto mchanga. Takriban watu 50 hawajulikani walipo lakini tunaendelea kupekua udongo, uwezekano wa kupata manusura ulikuwa mdogo kwani tukio hilo lilitokea saa 12 kabla waokozi hawajawasili eneo la tukio.

Mratibu wa jumuiya ya kiraia ya eneo hilo, Arsene Kasiama alisema maporomoko hayo pia yaliangukia watu waliokuwa wakinunua bidhaa sokoni na kuongeza kuwa manusura saba walijeruhiwa vibaya na zaidi ya watu 60 bado hawajapatikana.

 

DUWASA: Kasi ongezeko la Watu chanzo tatizo la Maji Dodoma
Parimatch yamtambulisha Haji Manara ‘El Bugati’