MkurugenziMkuu wa Mamlaka ya Ununuzi wa Umma Nchini (PPRA), Eliakim Maswi amekutana na Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Ununuzi wa Umma nchini Zimbabwe (PRAZ) kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika utendaji kazi kwenye eneo la ununuzi wa umma .

Akizungumza na Bodi hiyo April 15, 2024 jijini Dodoma iliyoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya PRAZ ,Maswi amesema pamoja na kutembelea ofisi za PPRA ,viongozi hao kutoka nchini Zimbabwe pia wametembelea Mji wa Serikali Mtumba , Ikulu na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kuangalia jinsi ambavyo Serikali ya Tanzania inafanya maana yote hayo yamefanyika kupitia ununuzi wa umma.

Amesema faida za ziara ya Wazimbabwe hao,Maswi amesema ni pamoja na kila mmoja kujifunza kutoka kwa mwenzake masuala ya ununuzi wa Umma.

“Mfano sisi tumeanza mfumo mpya wa ununuzi NeST ,mfumo huu sisi tumeusema na tumeutangaza kwa wenzetu,nadhani unakumbuka tulikuwa na watu wa Burundi hapa,lakini pia hapa tulipo tuna mwaliko kutoka Geibout wanataka nao tuwasaidie wawe kama sisi,tuna mwaliko kutoka Madagascar.

“Lakini wenzetu Wazimbabwe wamekuja kuona namna tulivyojenga mfumo sisi wenyewe na hivyo na wao wamekuja kuifunza katika eneo hilo ,kwa hiyo ni kitu kikubwa maana unapotangaza kuwa unafanya vizuri maana yake umefurahi,na sisi tunafarijika kwamba kumbe na wenzetu wanaweza kusikia kwamba Tanzania tunafanya wenyewe kazi ya kujenga mifumo,kwa hiyo ujio wao kwetu ni faida ,lakini pia si ndio urafiki tulio nao katika nchi za Afrika Mashariki na SADAC.”amesema Maswi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi nchini Zimbabwe, Ntombenhle Moyo amesema baada ya kujifunza nchini Tanzania namna ya kujenga mifumo hiyo nao wanakwenda kuwekeza katika eneo hilo.

Mkurugenzi Mtendaji uthibiti na ununuzi Umma PRAZ Clever Ruswa amesema,nchini Zimbabwe mfumo wao unajengwa na Mshauri Elekezi huku akisema baada ya kusikia nchini Tanzania mifumo inajengwa na watanzania wenyewe bila kutumia mshauri elekezi,wakaona waje wajifunze utaalam huo.

Ahmed Ally akataa unyonge mara mbili
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Aprili 16, 2024