Johansen Buberwa – Kagera.

Jeshi la Polisi Mkoani Kagera, linaendelea na uchunguzi wa kifo cha Mwanafunzi wa darasa la sita Shule ya msingi Kilima, Elius Antony (11),
mkazi wa Kijiji cha Kilima kilichopo Kata ya Nyakato Halmashauri ya Bukoba Mkoani Kagera, aliyekutwa ameuwawa na kutelekezwa kichakani na watu wasiojulikana.

Akitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari, Kamanda wa Polisi Mkoa Kagera, Blasius Chatand amesema tukio hilo lilitoke Aprili 10, 2024 na  Aprili 11, 2024 majira ya saa 17:00 jioni ndipo kijana huyo alikutwa ameuawa na mwili wake kutupwa kwenye pori la Kijiji cha Kilima, ukiwa na majeraha ya kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu ya shingoni, sikio la upande wa kushoto na kichwani.

Amesema, “baada ya kutekeleza mauaji hayo walichukua mfuko wa sandarusi wenye rangi ya njano aliokuwa nao marehemu ukiwa na unga wa mahindi kilo 2 ndani yake, simu moja aina ya Tecno pop 2 pamoja na pesa Sh 2500 ambayo ilibaki baada ya kulipa malipo ya kuchaji simu hiyo iliyokuwa chaji na mahemezi mengine nyumbani.”

Awali, Kmanda Chatanda alisema kabla ya umauti kumkuta marehemu, siku hiyo ya Tahere 10 akiwa na baba yake Antony Kaloli (42) wakiwa katika shughuli ya uchomaji mkaa katika kitongoji cha Mwizi, alimtuma mwanaye huyo aende nyumbani kuchukua unga na simu hiyo aliyokuwa ameiacha ikichajiwa dukani kwa Erneus Justinian, ndipo hakuonekana tena.

Masauni abainisha mafanikio ya Jeshi la Polisi
Ahmed Ally akataa unyonge mara mbili