Mkuu wa Majeshi ya Israel, Luten Generali Herzi Halevi ameapa kuchukua hatua za kulipiza kisasi dhidi ya Iran ambayo ilifanya shambulizi la kurusha zaidi ya makombora 300 na droni kuelekea Israel Aprili 14, 2024.

Hatua hiyo inafuatia hatua ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliongoza kikao cha baraza la vita la serikali yake ambacho kilijadili hatua zinazoweza kuchukuliwa kujibu shambulizi hilo la Iran.

Miongoni mwa hatua zilizojadiliwa na baraza hilo ni pamoja na kulenga kuweka usawa kati ya kusababisha uharibifu nchini Iran na si kuzusha vita vya kikanda.

Hata hivyo, Rais wa Marekani, Joe Biden na Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, David Cameron wamesema hawaungu mkono hatua hiyo ya kulipiza kisasi wakisema itazidisha maafa zaidi.

Bil. 743 zatolewa uwezeshaji Wananchi kiuchumi
Onana amaliza utata wa wazushi