Mlinda Lango wa Manchester United Andre Onana amesisitiza kuwa hajutii kuondoka Inter Milan na kuhamia Old Trafford mwanzono mwa msimu huu 2023/24.

Mlinda Lango huyo kutoka nchini Cameroon ametoa kauli hiyo baada ya kuonekana Uwanjani mwishoni mwa juma lililopita, akiifuatilia Inter Milan katika mchezo wa Ligi Kuu ya Italia, dhidi ya Cagriari iliyokubali kulazimishwa sare ya 2-2.

Onana amesema suala la kuondoka Inter Milan lilikuwa sehemu ya mipango yake tangu mwishoni mwa msimu uliopita, hivyo anapaswa kuheshimiwa kwa maamuzi hayo, na katu hajutii maamuzi yake.

“Nina furaha nilipo. Lakini nina furaha sana kuitazama Inter kila inapocheza, ni timu nzuri yenye wachezaji wa ajabu na kocha bora. Inafurahisha kufikiria tulichofanikisha pamoja msimu uliopita.

“Inter ni familia kwangu, ninawapenda mashabiki. Nawatakia kila la kheri. Je, unajuta? Hapana, nina furaha nikiwa Manchester United. Lakini nina furaha kwa Inter, klabu ni ya ajabu, na timu hii ni nzuri.”

“Sitaweza kwenda Italia mara kwa mara, kwa nilikwenda kuwapongeza. Ni wakati wa kihistoria kwa Inter, na nina furaha sana kwa timu hiyo, ambayo imefanya kazi vizuri sana msimu huu. Natumai wataendelea kushinda katika miaka michache ijayo.” amesema Onana

Klabu ya Manchester United ilithibitisha kumsajili Onana 20 Julai 20 mwaka 2023, kwa ada ya awali ya Pauni Milioni 43.8, na kuna uwezekano wa kuongeza Pauni Milioni 3.4 mwishoni mwa msimu huu.

Onana alicheza mchezo wa kwanza akiwa na Man Utd dhidi ya Wolverhampton Wanderers mwanzoni mwa msimu huu 2023/24.

Israel wajifungia kuijadili Iran, wasema itajuta
Gamondi: Simba SC hainipi Presha