Shirikisho la Soka nchini Saudi Arabia (SAFF) litakagua upya kanuni za maadili kwa mashabiki baada ya shabiki mmoja kuonekana akimchapa viboko mchezaji wa klabu ya  Al-Ittihad.

Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa mechi baada ya Al-Ittihad kufungwa na Al-Hilal katika michuano ya Saudi Super Cup mjini Abu Dhabi.

Picha na Video zinaonyesha mshambuliaji wa Al-Ittihad, Abderrazak Hamdallah akimrushia maji shabiki, ambaye kisha anampiga mchezaji huyo mara mbili kwa kile kinachoonekana kama mjeledi.

SAFF ilisema “Tumeshtushwa na matukio ya aibu. Kandanda nchini Saudi Arabia ni mchezo wa familia na tunashukuru, machafuko ya mashabiki ni nadra sana,”

“Ndio maana vitendo vya shabiki huyu vinaenda kinyume na yote ambayo soka la Saudia linawakilisha na tunalaani vikali tukio hilo.

“Kutakuwa na ukaguzi wa kina wa maadili ya mashabiki. Ukaguzi huo utahakikisha sheria na kanuni zilizoboreshwa zinawekwa ili kutoa adhabu kwa haraka ili kuzuia kurudiwa kwa matukio kama haya.” SAFF ilisema.

Chanzo: BBC Swahili

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Aprili 17, 2024
Rais La Liga afichua majanga FC Barcelona