Johansen Buberwa – Kagera.

Takriban Wasichana 20,759 walio chini ya umri wa miaka 14 katika Halmashauri Wilaya Missenyi Mkoa Kagera, wanatarajia kupatiwa Chanjo ya HPV, ili kuwakinga dhidi ya ugonjwa wa Saratani ya shingo ya mlango wa kizazi.

Akizungumza kwenye kikao cha kujadili namna ya zoezi hilo Mratibu wa huduma za chanjo Halmashauri ya Wilaya Missenyi, Edward Kagari amesema wanatarajia kutumia dozi elfu21,000 kwenye zoezi hilo litakaloanza Aprili 22 – 28,2024 kwa wasichana waliyopo chini ya umri wa miaka 9 hadi 14.

Afisa mpango wa chanjo na Mratibu wa shughuli za shirika za la JHPIEGO Tanzania, Emmanuel Tesua amesema kupitia mradi wa MCGL unaofadhiliwa na USAID katika Wilaya zote za Mkoa wa Kagera watahakikisha wanatoa hamasa ya kufanikisha zoezi hilo.

Awali Mwenyekiti wa Kikao hicho ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Missenyi, Kanali mstaafu Hamis Maiga akifunguA kikao hicho amehimiza Viongozi mbalimbali wakiwemo Watendaji wa Kata, Vijiji, Viongozi wa dini na Wataalamu wa afya kuhakikisha wanatoa hamasa ya upatikanaji kwa walengwa kwenye maeneo yao ili waweze kupatiwa chanjo hiyo.

Chanjo ya HPV inayotumika kwa ajili ya kutoa Kinga dhidi virusi vya HPV vinavyosababisha saratani ikiwemo ya mlango wa shingo la kizazi ambapo Shirika la afya Duniani (WHO) limeidhinisha Nchini Tanzania mwaka 2014 na kuanza kutumika mwaka huo kwa kuanzia Mkoa wa Kilimanjaro kwa Wasichana ambao walio chini ya umri wa miaka 14 kwa kuwapatia dozi mbili.

TAWA yawashika mkono waathiriwa wa mafuriko Rufiji
Anthony Martial kuondoka Man Utd