Sakata la Mshambuliaji kutoka nchini Zimbabwe Prince Dube na Uongozi wa Azam FC linatarajiwa kuwa sehemu ya mshauri yatakayopitiwa na Kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji na wanachama ya TFF iitakayotana kesho Alhamisi (April 18).

Dube ameamua kujiweka mbali na Azam FC, kufuatia kuomba kuvunja mkataba na Uongozi wa Azam FC siku kadhaa zilizopita, na jambo kubwa linalopingwa mbele ya kamati hiyo ni madai ya kuwepo kwa mkataba baina ya pande hizo  mbili hadi mwaka 2026.

Dube aliiandikia TFF kulalamika kuhusiana na mkataba mpya wa Azam FC kwamba kuna vitu haviko sawa kwahiyo hautambui mkataba huo.

Dube anadai hadi anaondoka klabuni hapo alikuwa na mkataba na Azam FC hadi Julai 24, 2024 na ndipo unapaswa kuanza mwingine wa miaka 2 ambao utafikia tamati Julai 2026.

Katika kesi hiyo itakayoanza kusikilizwa kesho Alhamisi (April 18), Azam FC watawakilishwa na wakili wa kimataifa kutoka Ureno na ameshawasiliana na TFF kuona uwezekano wa shauri la Prince Dube kufanyika kwa njia ya mtandao (zoom meeting) ili aweze kushiriki akiwa huko huko Ureno, wawakilishi wa Dube bado haifahamiki wanatokea wapi.

Usafirishaji Korosho ghafi umelipa Bandari ya Mtwara
Madini ya Dolomite yawainua Wananchi kiuchumi Handeni