Mbunge wa Jimbo la Kibamba, Issa Mtemvu leo April 22, 2024 akiwa Bungeni jijini Dodoma ameihoji Serikali ieleze ina kauli ipi juu ya kutokamilika kwa Miradi ya Maji katika Jimbo la Kibamba.

Swali hilo limejibiwa na Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew ambapo amesema Serikali imekamilsha ujenzi wa miradi mitatu ya Mradi wa Usambazaji Maji kutokea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hadi Bagamoyo (2B-2F), Mshikamano na Kitopeni.

Amesema, miradi hiyo inanufaisha wakazi wapatao 210,876 wa Jimbo la Kibamba.

Liverpool kuivurugia Man Utd kwa Mikayil Faye
13 wafariki kwa ajali ya Coaster kugongana na Roli