Aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Chelsea na Man Utd Jose Mourinho amemuonya Kocha Mkuu wa Arsenal Mikel Arteta, akimtahadharisha kuhusu mbinu anazozitumia katika kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa msimu huu 2023/24.

Arsenal ni sehemu ya timu tatu zinazowania Ubingwa msimu huu, ikiwa kileleni kwa sasa kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa dhidi ya Liverpool, huku zote zikiwa na alama 74, mbele ya Man City yenye alama 73 ikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Mourinho amesema Arteta anatakiwa kujitafakari sana na mbinu zake, kwani haoni kama zinaweza kuleta miujiza katika mbio za ubingwa, hivyo hana budi kujipanga kivingine ili kufikia malengo aliyojiwekea klabuni hapo.

Kocha ambaye pia aliwahi kuzinoa klabu za Inter Milan, Roma, Real Madrid, Porto na Tottenham ametolea mfano wa jinsi Arsenal walivyojihami kwa sare dhidi ya Manchester City mapema msimu huu.

Mourinho anahisi kwamba Arteta alisifiwa sana kwa mbinu hizo, ingawa mara nyingi anakosolewa kwa kuanzisha timu zake kwa kujilinda sana.

“Nina furaha kwa sababu nampenda mtoto. Na nina furaha kila kitu kinakwenda kwa ajili yake. Lakini jinsi (Arsenal) walivyocheza kupata hatua hiyo na jinsi vyombo vya habari vilizungumza kuhusu mkakati wa kimaajabu.

“Katika wakati wangu, haikuwa mkakati wa kimaajabu. Na niliishinda Manchester City mara chache. Lakini haikuwa mkakati wa ajabu. Ulikuwa ni mchezo wa kujilinda. Ulikuwa ni mtazamo tofauti.

“Wana mabeki wangapi wa kati kwenye timu? Wakati mwingine wana sita, kama kanuni, halafu wanacheza nafasi zingine. Wanacheza beki wa kulia, kushoto, kiungo, lakini wanacheza na watano au mabeki sita wa kati uwanjani wanahisi hitaji la uimara wa safu ya ulinzi na uimara wa ulinzi.” amesema Mourinho alipohojiwa na Gazeti la The Telegraph

Ikumbukwe kuwa Arsenal leo Jumanne (Aprili 23) itakuwa nyumbani Emirates Stadium kuikaribisha Chelsea katika mchezo wa Mzunguuko wa 34 wa Ligi Kuu ya England.

Barabara ya Jangwani yafungwa, huduma mwendo kasi zasimama
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Aprili 22, 2024