Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo amesema kampeni maalum iliyoendeshwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania – TIC, ililenga kutoa elimu ya uwekezaji kwa Wananchi, ikiwemo kuondoa dhana kuwa ili kuwekeza nchini lazima uwe mgeni na kwamba katika eneo hilo hatua zimepigwa na inaonekana.

Prof. Mkumbo ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano maalum na Dar24 Media na kuongeza kuwa kupitia utekelezaji wa sera na sheria mbalimbali za uwekezaji na maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Serikali imeendelea kupata mafanikio mbalimbali katika kuhamasisha, kuvutia na kuwezesha uwekezaji nchini.

Amesema, “mwaka 2024 ni mwaka wa kitaifa wa kuhamasisha uwekezaji nchini kutakuwa na fursa ya kueleza taratibu za kusajili miradi ya uwekezaji kupitia TIC, kueleza vivutio mbalimbali vya kikodi na visivyo vya kikodi vinavyotolewa kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wanaposajili miradi yao.”

Prof. Mkumbo amesema fusra nyingine ni pamoja na kusikiliza, kupokea na kutatua changamoto zinawakabili Watanzania katika uwekezaji na mazingira ya biashara kwa ujumla, kuongeza wigo wa uelewa kuhusu dhana na taratibu za uwekezaji nchini.

TAKUKURU yaibua madudu ukusanyaji kodi Manyara
Ndejembi: Wasiojisajili OSHA hawatovumiliwa