Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU, Mkoa wa Manyara imeokoa shilingi Miliomi 44.36 ambazo zilikusanywa kwa mashine na POS bila kupelekwa benki kwa kipindi cha miezi nane.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Manyara, Suzan Raymond amesema kati ya fedha hizo shilingi 29,181,000 zilikusanywa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto bila kupelekwa benki.

Amesema shilingi 8,064,474 ni kodi ya zuio ambazo zilipelekwa TRA baada ya uchunguzi wa TAKUKURU na kwamba pia waliokoa shilingi 7,120,000 ambazo ni mshahara wa mtumishi hewa, aliyeajiriwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.

Suzan amesema, fedha hizo zilizuiwa benki wakati wa uchunguzi wa sakata la watumishi hewa tangu wakati wa oparesheni ya kusaka watumishi hewa kipindi cha Serikali ya awamu ya tano.

Wachimbaji Wadogo wamuamsha Waitara Bungeni
Uwekezaji: Hatua zimepigwa na tunaona - Prof. Mkumbo