Watanzania wametakiwa kutumia fursa za wasaidizi wa msaada wa kisheria, ili kupata huduma za kisheria na kutatua migogoro inayowakabili katika maeneo yao.

Wito huo, umetolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko hii leo Mei 26, 2024 Mkoani Njombe, katika hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia.

Amessma, Serikali iliamua kuandaa Kampeni hiyo ili kusaidia wananchi wasio na uwezo wa kumudu gharama za kisheria kupata huduma hizo bila malipo na kutatua changamoto zao.

Dkt. Biteko ameongeza kuwa, ili kuwa na jamii ya watu wenye kuelewana ni muhimu kutatua migogoro mapema ili kuepusha madhara yanayosababishwa na migogoro hiyo ikiwemo visasi.

Aidha, amewataka wasaidizi wa msaada wa kisheria kuhudumia wananchi kwa kusikiliza kero na migogoro inayowakabili kwa upendo huku akiitaka Wizara ya Katiba na Sheria kutekeleza jukumu la kusaidia upataji wa huduma za sheria kwa kuimarisha matumizi ya mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), ili wananchi wasisafiri umbali mrefu kutafuta haki.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Mei 27, 2024
CCM Kibaha wataka Rais Samia aendeleze alipoishia