Scolastica Msewa, Kibaha – Pwani.

Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi – CCM, Mkoa wa Pwani, David Mramba amesema katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 watatqmbua fomu moja tu ya kuomba kugombea Uongozi wa nafasi ya urais ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, ili aendeleze kasi ya alipoishia kwenye utekezaji wa miradi ya maendeleo nchini.

Mramba ametoa rai hiyo aliyakutanisha mashirika 22 yasiyo ya kiserikali ambayo yanamrengo mmoja wa kukisemea chama na Serikali na kusisitiza uzalendo kwa Wananchi, ambayo yanazofanya kazi zake katika Mkoa wa Pwani.

Amesema katika Mkoa huo ipo miradi mingi imetekelezwa na inahitaji kuendelezwa na kukamilishwa hivyo kutokana na hali hiyo katika uchaguzi kuu fomu ya Rais kutoka chama hicho itakuwa kwa ajili mgombea mmoja pekee wa nafasi ya urais.

“Mwingine yeyote atakayechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo hatutamtambua ili malengo ya kimkoa na taifa yatimie,” alisema Mramba.

Aidha, Mramba aliyataka mashirika hayo  kuhakikisha hayatumiki kama kichaka cha maovu kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na malengo ya uanzishwaji wake.

Dkt. Biteko. Msaada wa kisheria uwasaidie Watanzania
Ajali ya Mtumbwi yauwa saba Katavi