Swaum Katambo – Katavi.

Takriban Watu saba wameaga dunia, baada ya Mtimbwi waliokuwa wakisafirisha magunia ya mpunga katika bonde dogo la Kitongoji cha Luguya kilichopo Kijiji cha Mwamapuli Halmashauri ya Mlele mkoani Katavi kupinduka.

Akitoa taarifa ya tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Katavi, Inspekta Lilian Wanna amesema tukio hilo limetokea mei 24 majira ya saa 12 jioni na watu hao ji miongoni mwa 14 waliokuwa kwenye Mtumbwi huo.

Amesema, ajali hiyo iliwakuta watu hao walipokuwa wakitoa mazao yao shambani baada ya kuyavuna ili kuyaleta kijijini na kwamba bado wanaendelea na zoezi la uokoaji, licha ya kuwa bonde hilo kuwa na changamoto ya uwepo Wanyama wakali kama Mamba na Viboko.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama, Mwanamvua Mrindoko amefika kijijini hapo kutoa pole kwa wafiwa na kuwataka Wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Zimamoto katika kazi ya uokoaji.

CCM Kibaha wataka Rais Samia aendeleze alipoishia
Mchengerwa awagusa wanaofanya kazi kwenye mazingira magumu