Wakurugenzi wa Halmashauri nchini wametakiwa kuhakikisha Watumishi wote wanaofanya kazi kwenye mazingira magumu wanapata stahiki zao kwa wakati.

Agizo hilo, limetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa wakati akizungumza na baadhi ya watumishi na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi pamoja na wananchi katika ziara yake wilayani humo.

Amesema, “nimejionea watumishi wanavyofanya kazi kwenye Hospitali ya wilaya ya Malinyi, wanafanya kazi kwa moyo, wanajitoa kuwahudumia watanzania sasa watumishi kama hawa na wale walioko kwenye maeneo mengine ya namna hii wasîkatishwe tamaa kwa kucheleweshewa stahili zao wapewe kwa wakati.”

Aidha, Mchengerwa ameongeza kuwa, “Watumishi niendelee kuwatia moyo kuwa kazi mnayofanya ya kuwahudumia watanzania ni ya muhimu sana kwa Taifa letu mnahakikisha wananchi hawa wa pembezoni kupata huduma bora kama wale wa mjini niwahakilishie hapa mnapata thawabu kwa Mungu.”

Ajali ya Mtumbwi yauwa saba Katavi
Zelensky: Putin anatakiwa kujitafakari