Gavana wa mji wa Kharkiv Nchini Ukraine, Oleh Syniehubov amesema Mabomu mawili ya kutelekezwa, yamewauwa takribani watu 11 na wengine ambao idadi yao haijafahamika mara moja kujeruhiwa, baada ya vikosi vya Urusi kushambulia duka moja katika mji huo.

Akizungumzia tukio hilo Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amesema inakadiriwa kuwa zaidi ya watu 200 huenda walikuwa ndani ya duka hilo kubwa wakati shambilizi likitokea.

Amesema shambulio hilo ni udhihirisho tosha juu ya mauaji ambayo yanafanywa na Urusi dhidi ya raia wake wasio na hatia na kusema Putin anapaswa kutafakari juu ya hayua anazozichukua.

Awali ilisemekana watu sita walifariki papo hapo na wengine 40 walijeruhiwa huku 16 wakiwa hawajulikani waliko, ambapo pia Meya wa Kharkiv, Ihor Terekhov alisema tukio hilo ni la kigaidi.

Mchengerwa awagusa wanaofanya kazi kwenye mazingira magumu
Israel, Hamas nani mkweli? ndugu wataka Netanyahu ajiuzulu