Abel Paul, Jeshi la Polisi – Dar es Salaam.
Jeshi la Polisi Kikosi cha kupambana na kuzuia wizi wa mifugo nchini, kimesema kimeendelea kutoa elimu kwa wafugaji na makundi mengine ya wananchi kitendo kilichopelekea kukamatwa kwa mifugo ipatayo thelathini na nane iliyokuwa ikitoroshwa Kwenda nchini Jirani.
Akitoa taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Simon Pasua amesema kikosi hicho kimefanikiwa kukamata mifugo 38, pamoja na watuhumiwa waliokuwa wakitorosha mifugo hiyo Kwenda nchi Jirani.
Kamanda Pasua amebainisha kuwa, kikosi hicho kinaendelea kutoa elimu kwa wafugaji ambapo imesadia kuongeza idadi ya mifugo inayoingia katika machinjio ya kimataifa ya kiwanda cha Elia Food kilichopo Namanga wilaya ya Longido Mkoani Arusha.
Aidha, Kamanda Pasua pia ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa wazalendo kwa kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi juu ya watu wachache wanajihusisha na utoroshaji wa mifugo hapa nchini.