Wafanyakazi 597 wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) waliofutwa kazi wataanza kulipwa stahiki zao kuanzia kesho, (Aprili 13).

Kaimu Mkurugenzi wa NIDA, Modestus Kipilima ameeleza katika taarifa yake jana kuwa Mamlaka hiyo itaanza kuwalipa wafanyakazi wake kwa mgawanyo wa awamu tatu.

Akitaja migawanyo hiyo iliyopo katika makundi kulingana na kazi walizokuwa wanafanya watumishi hao, alibainisha kuwa kundi la mwisho litakamilishiwa malipo Aprili 17 mwaka huu.

NIDA ilitangaza kuwafutia mkataba watumishi hao Machi 7 mwaka huu kwa kile ilichodai kutokuwepo kwa uhaba wa fedha na vitendea kazi visivyowatosheleza.

Wafanyakazi hao walilalamika wakidai kusitishiwa mkataba bila kufuata taratibu za kisheria pamoja na kutolipwa stahiki zao.

Anne Kilango asema haya baada ya Rais Magufuli kumtimua ‘Ukuu wa Mkoa’
Dk. Slaa: Tutaheshimiana tu