Promota Eddie Hearn, amemtahadharisha bondia kutoka nchini England Amir Khan, kwa kumwambia kama anahitaji kuendelea kuwa juu kibiashara itamlazimu kumchakaza mpinzani wake Manny Pacquiao.

Hearn ametoa tahadhari hiyo akifahamu fika mpambano wa wawili hao uliopangwa kufganyika April 09 mjini Las Vegas, nchini Marekani utakua na upiznani mkali kutokana na kila mmoja kuhitaji kushinda.

Amesema Khan bado ana nafasi kubwa ya kuendelea kupambana katika masumbwi tofauti na Manny Pacquiao, hivyo kama atahitaji kuendelea kuwa kigezo kizuri kwa wengine anapaswa kufanya kweli katika mchezo huo ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa masumbwi duniani kote.

Mchezo huo, huenda ukawa wa mwisho kwa Manny Pacquiao, ambaye alitangaza kuwa mbioni kuachana na mchezo wa masumbwi, na alidiriki kuutaja mwaka 2016 kuwa wa mwisho katika himaya ya kutamba katika mchezo huo.

Khan anajiandaa kwenda katika mchezo huo wa April 09, huku akibebwa na rekodi ya kushinda mapambano 31 ambapo kati ya hayo aliyowatoa nishai wapinznai wake kwa KO ni 19 na ameshindwa matatu.

Perez Kuingia Vitani Dhidi Ya Benzema
Garde: Nimeshawishiwa Na Gerard Houllier