Klabu ya Real Madrid imetoa taarifa za kusikitishwa na tukio la kukamatwa kwa mshambuliaji wao, Karim Benzema kufuatia tuhuma za uvujishaji wa picha chafu za video zinazo muhusu mshambuliaji wa klabu ya Olympic Lyon, Mathieu Valbuena.

Uongozi wa klabu hiyo, umesisitiza kutopendezwa na tukio hilo ambalo lilijitokeza siku ya jumatano nchini Ufaransa, hali ambayo kwao wamalipokea kama udhalilishaji kwa mchezaji wao.

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo ya mjini Madrid imeeleza kwamba, uongozi wa The Galacticos umeapa kulivalia njuga suala hilo hadi kuona mwisho wake.

Dhamira kubwa ya kusisitiza hivyo, ni kutaka kumuona mshambuliaji wake akiwa huru na aweze kurejea katika majukumu yake ya kazi kama ilivyo ada.

Katika hatua nyingine rais wa Real Madrid, Florentino Pérez, alielekea nchini Ufaransa kwa lengo la kukutana na Benzema na kwa bahati nzuri jambo hilo limefanikiwa.

Perez ameahidi kuwa sambamba na Benzema, na amemuhakikishia kupigana kufa na kupona ili kulimaliza jambo linalomkabili, ambalo huenda likawa sababu ya kumuondoa katika kasi yake ya upachikaji mabao.

Kasi Ya Rais Magufuli Yaanza Kuwanyoosha Hawa
Amir Khan Apewa Ushauri Wa Bure