Mwanamuziki wa bongo fleva Whozu na video Vixen Tunda, miezi mitatu tangu waonyeshe mapenzi yao katika mitandao ya kijamii, imeonekana penzi la wawili hao limeingia dosari baada ya tunda kuonekana akimuomba msamaha Whozu.
Tunda amechapisha picha ya kekei katika mtandao wa kijamii wa instagram amabyo imendikwa ”am sorry” kisha kuandika ujumbe unaoeleza jinsi alivyo jutia kumkosea Whozu.
”Najichukia mimi mwenyewe kwasababu nimemuumiza mtu muaminifu, mzuri, anayenijali ambaye sijawahi kumjua kabla , kama unaweza naomba unisamehe bado nakuhitaji kwenye maisha yangu, nimefanya vitendo vya kitoto najionea aibu kwa tabia yangu naomba unisamehe, penzi lako ni msukumo wangu usiniache. Kwangu ni fahari kuwa na wewe, nakupenda na unisamehe Whozu”, ameandika Tunda.
Hata hivyo baada ya mrembo huyo kuandika hivyo Whozu hakujibu chochote, hata katika mtandoo kijamii wa instagram ambao Tunda hajamfuata mtu yeyote kwenye mtandao huo.
- Prof Jay atuma salamu nzito kwa wasanii wa HipHop
- MC Pilipili atangaza nia ya kuwania ubunge, ataja chama