Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kupata ajali leo jioni.

Taarifa za awali zimeeleza kuwa Dk. Tulia amepata ajali hiyo baada ya gari dogo kugonga gari alilokuwa akisafiria katika eneo la Kiwira jijini Mbeya akielekea Tukuyu.

Chanzo chetu cha uhakika kimeeleza kuwa dereva na abiria wote waliokuwa kwenye gari hilo pamoja na Naibu Spika huyo wako salama japo gari lao limeharibika vibaya.

Tutakujuza habari zaidi kuhusu ajali hiyo na tunamuombea Dk. Tulia awe mzima kama zamani.

Wasira ageuka Mbogo, ajaribu kumgonga na gari mwandishi, kumpokonya kamera
Video Mpya: Nzaya Don Ngosha Ft. Mirror - Achana na Mimi