Mayenga ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM), aliweka wazi ombi lake kwa Rais Magufuli hivi karibuni alipokuwa akizungumza katika kikao cha Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), mkoani Shinyanga. Alisema kuwa chanzo cha ombi lake ni majukumu mengi yanayomkabiri na kwamba anataka ajikite zaidi katika kusimamia biashara zake binafsi pamoja na majukumu ya ubunge.
“Ombi hili nililitoa binafsi kwa Waziri Mkuu ambaye alinishauri kusubiri uteuzi; isitafsiriwe kwamba nimeogopa kasi ya utendaji ya Serikali ya Awamu ya Tano.Hapana! Nimeona ni vyema nibaki na ubunge na biashara zangu,” alisema.
Mayenga ni mwandishi wa habari kitaaluma na amekuwa Mkuu wa Wilaya wa Kwanza kuweka hadharani kutokuwa na nia ya kuendelea na wadhifa huo kwenye serikali ya awamu ya Tano.