Mshambuliaji wa klabu ya KRC Genk ya Ubeligiji na timu ya timu ya Taifa Tanzania, Mbwana Ally Samatta, Jumatano atakiongoza kikosi cha Taifa Stars kama Nahodha katika mchezo dhidi ya Chad.

Samatta aliteuliwa kuwa Nahodha mpya wa Taifa Stars Januari mwaka huu na kocha Mkuu Charles Boniface Mkwasa, akirithi mikoba ya Nadir Haroub.

Nahodha huyo mpya aliyeteuliwa kuwaongoza wenzake uwanjani na kocha mkuu Charles Mkwasa, alikuwa mchezaji wa kwanza kuwasili D’jamena – Chad siku ya Jumamosi tayari kwa mchezo huo.

Jukumu la Samatta ni kuhakikisha anawaongoza kupata ushindi wachezaji wenzake katika mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa AFCON dhidi ya wenyeji, pia kuidhihirishia dunia kuwa yeye ni mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani mwaka 2015.

Tangu ajiunge na klabu ya KRC Genk inayoshiriki Ligi Kuu nchini Ubelgiji, Samatta amefanikiwa kuziona nyavu za wapinzani mara mbili, hivyo ana jukumu kubwa kama nahodha kuisaidia timu yake ya Taifa kuibuka na ushindi dhidi ya Chad akiwa kama nahodha na mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani.

Joe Hart Na Raheem Sterling Waondolewa Timu Ya Taifa
Mkuu wa Wilaya amuomba Magufuli amuondoe