Imeelezwa kuwa Klabu ya Young Africans imeachana na mpango wa kumsajili Kiungo kutoka nchini Burundi na klabu ya Kiyovu FC ya Rwanda Abeid Bigirimana, ambaye alikua anapewa nafasi kubwa ya kutua Jangwani mwishoni mwa msimu huu.

Kiungo huyo ambaye kwa sasa ni Moto wa Kuotea mbali katika Ligi Kuu ya Rwanda, aliwekwa kwenye mipango ya Young Africans kwa matarajio ya kusajiliwa kutokana na uwezo wake, lakini gharama yake ya usajili inatajwa kuwa kikwazo.

Habari zinasema kwamba Kiyovu FC baada ya kuona Young Africans wana uhitaji mkubwa kwa mchezaji huyo walishikilia msimamo wa kutaka zaidi ya Sh350 milioni za Tanzania ambazo klabu hiyo haipo tayari kutoa kwa mchezaji mmoja.

“Huyu mchezaji gharama yake imekuwa kubwa sana mpaka viongozi wakasema wakienda DR Congo wanaweza kupata wachezaji zaidi ya mmoja kwa hiyo gharama,” amedokeza mmoja wa viongozi wa Young Africans.

Kocha Msaidizi Cedrick Kaze na Mjumbe wa kamati ya Usajili ya Young Africans Hersi Saidi waliwahi kutajwa kwenda nchini Rwanda kumfuatilia Bigirimana.

Young Africans ambayo inataka kusuka kikosi chake mapema tayari kwa michuano ya kimataifa badae mwaka huu ilimtaka Bigirimana kama mbadala wa Sureboy ambaye anacheza staili ya ‘Box kwa box mwenye mapafu ya mbwa’

Kiufundi usajili wa Bigirimana ulimaanisha benchi la ufundi la timu hiyo lilitaka kuimarisha kiungo cha kati ambacho kwa sasa anacheza Khalid Aucho, Abubakar Salum ‘Sure Boy’, Zawadi Mauya na Yannick Bangala.

Joash Onyango mambo safi Simba SC
Ahmed Ally awaita mashabiki Kwa Mkapa