Katika kuendeleza kauli mbiu isemayo, “Kila ujauzito unahitajika na kila uzazi ni Salama,” Shirika la Umoja wa Mataifa la Maswala ya Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu UNFPA leo wamekabidhi kwa Serikali, bidhaa za Afya ya Uzazi kupitia Wizara ya Afya.

Msaada huo umekabidhiwa wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Hali ya Idadi ya Watu Duniani (SWOP) yaliyofanyika katika bohari ya dawa MSD, na Mwakilishi mkazi Shirika la Umoja wa Mataifa la Maswala ya Afya ya Uzazi UNFPA, Mark Bryan Schreiner.

Schreiner amesema, lengo ni kutambua lengo letu la pamoja la kuhakikisha kuwa wanawake, wanaume, na vijana wote nchini Tanzania wanapata bidhaa za uzazi wa mpango, bila kumuacha mtu nyuma.

Vifaa vya afya ya uzazi vilivyokabidhiwa na UNFPA kwa Serikali ya Tanzania ni bidhaa za kuokoa maisha ya uzazi zikiwemo bidhaa za kisasa za uzazi wa mpango.

“Bidhaa hizi ni zana kwa watu binafsi kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi juu ya afya zao za uzazi, pindi na wakati sahihi wa kupata watoto. Vifaa hivi vinatoa njia za uwezeshaji binafsi, hasa Kwa wanawake na wasichana,” amesema Mark.

Ameongeza kuwa lengo la pamoja ni usambazaji wa dawa za uzazi wa mpango na vifaa vya afya ya uzazi kwa maelfu ya vituo vya afya, hospitali, zahanati na huduma za kijamii, kisha kusambazwa ili kutoa haki na chaguo za upangaji uzazi kwa wanawake na wanaume kote nchini.

Mwakilishi mkazi Shirika la Umoja wa Mataifa la Maswala ya Afya ya Uzazi UNFPA, Mark Bryan Schreiner

“Tunaipongeza Serikali ya Tanzania kwa dhamira ya FP2030 ya kuendeleza uzazi wa mpango unaozingatia haki, na ongezeko lililopangwa la 10% la kila mwaka katika mgao wa sasa wa Shilingi bilioni 14 za Tanzania zitakazotolewa kikamilifu kwa ajili ya ununuzi wa vidhibiti mimba,” ameongeza.

Aidha Mark ameongeza kuwa kupitia ushirikiano wa UNFPA wa Ugavi, ushirikiano utaendelea zaidi na Serikali ya Tanzania mwaka huu ili kuanzisha maelewano ya nchi na kuimarisha dhamira ya pamoja ya ufadhili wa siku zijazo kwa ajili ya vifaa vya afya ya uzazi.

“Katika makabidhiano haya ya kihistoria, tunaadhimisha ununuzi wa bidhaa za afya ya uzazi ulofanywa na UNFPA kufikia thamani ya dola za kimarekani milioni 4.6 kwa mwaka huu wa 2022,” amebainisha Mark.

Am,eongeza kuwa, “zaidi ya dola milioni 4 zinatoka kwa Ugavi wa UNFPA na zaidi ya dola 500,000 zinatoka Ofisi ya Maendeleo ya kimataifa na Jumuiya ya Madola ya Uingereza. (FCDO).”

Kuanzia 2015 hadi 2021 UNFPA na FCDO zimenunua 53% ya bidhaa za afya ya uzazi nchini Tanzania.

Jumla ya thamani ya bidhaa hizi ni dola za Kimarekani milioni 54.2, ambapo zaidi ya milioni 24.8 zilitoka kwa FCDO na milioni 29.4 kutoka kwa Ugavi wa UNFPA.

Tunakadiria kuwa bidhaa hizi zitapunguza mimba zisizotarajiwa milioni 9, kuzuia vifo vya karibu milioni moja vya uzazi, kuzuia utoaji mimba usio salama milioni 2, na kuokoa dola za Marekani milioni 756 katika huduma ya moja kwa moja ya afya.

Matokeo ya Mabadiliko ya UNFPA ni pamoja na kufikia Asilimia sufuri ya uhitaji wa njia za uzazi wa mpango na Vifo vya uzazi vinavyoweza kuzuilika.

UN yataka uchunguzi vifo 23 vya Waafrika
Ajali ya ndege Somalia, 30 wanusurika kifo